Na. Elinipa Lupembe.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha A to Z Textile Mills Limited cha Arusha, Binesh Haria na familia yake wamekabidhi chumba kimoja cha darasa, shule ya sekondari Mateves halmashauri ya Arusha, darasa walilojenga shuleni hapo, kama ishara ya kumbukizi ya wapendwa wao, Vilas J. Shah na Nathalal Hirji Shah waliotangulia mbele za haki miaka kadhaa iliyopita.
Akizungumza kwa niaba ya famili ya bwana Binesh, wakati wa kukabidhi darasa hilo, katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, mkurugenzi wa kiwanda cha A to Z, Sylevester Kazi, amesema kuwa, licha ya kuwa familia ya Binesh kujenga darasa hilo kama kumbukizi ya wapendwa wao, lakini lengo kubwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita, ya kuboresha miundombinu ya elimu na kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira bora wakati wote wawapo shuleni.
Amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii kwa kuwa, tayari serikali na wadau wanafanya juhudi za kuwaandalia mazingira rafiki ya kujifunzia, mazingira ambayo yanahitaji mwanafunzi mwenyewe kufanya jitihada binafsi ili aweze, kujifunza na hatimaye kufaulu vizuri katika matokeo ya mitihani yake.
"Kujifunza ni haki ya kila mtu, kila mtu aliyezaliwa amepewa uwezo wa kujifunza, tumieni zawadi hiyo kwa kuongeza jitihada binafsi ili kupata utalamu ambao kila mwanafunzi hapa anamatamanio ya kuwa mtalamu wa fani fulani, wapo wanaotaka kuwa madaktari, wahandisi, walimu, marubani n.k, ili kupata utalamu na kufikia matamanio hayo, zinahitajika jitihada binafsi katika masomo yenu mkiwa hapa shuleni" amesisitiza Kazi
Hata hivyo Kazi ameweka wazi kuwa, Mkurugenzi wa kiwanda cha A to Z, bwana Binesh, amekubali ombi la mkuu wa shule ya sekondari Mateves, kuwa mlezi wa shule hiyo kuanzia sasa, pamoja na kutoa ahadi ya kuongeza kujenga matundu ya vyoo vya shule hiyo, ujenzi ambao utaanza mapema mara baada ya mchakato wa ujenzi kukaa sawa.
Naye Mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha, Selemani Msumi ameishukuru familia ya Bwana Binesh na uongozi wa kiwanda cha A to Z Textile kwa kujitoa, kwa kuunga mkono juhudi za serikali pamoja na kuona umuhimu wa watoto wa kitanzania kusoma katika mazingira bora.Aidha mkurugenzi Msumi amewataka wanafunzi kutunza miundo mbinu hiyo kwa ili ilweze kutumika vizazi na vizazi na kuwasisitiza kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao huku akiwataka walimu kuwasimamia wanafunzi hao katika kutunza miundombinu ya madarasa pamoja na kuwaongoza kujifunza kwa bidii na kupata ufaulu mzuri.
Mkurugenzi Msumi amewataka wadau wa maendeleo ndani na nje ya halamshauri, kuendelea kujitokeza katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita, katika kuboresha sekta ya elimu, na kusisitiza kwamba serikali iko tayari kufanya kazi na wadau kwa kuweka mazingira bora na rafiki kwao.
Mkuu wa shule ya sekondari Mateves, mwalimu Sayuni Tarimo, ameushukuru uongozi wa kiwanda cha A to Z kupitia mkurugenzi Binesh, kwa kujenga darasa pamoja na kukubali kuwa mlezi wa shule hiyo, jambo ambalo mkuu huyo wa shule ameliita ni la kiungwa na anategemea kupitia bwana Binesh, taaluma ya shule ya Mateves itapandisha.
Shule ya sekondari Mateves ni moja ya shuze za kata inayokua kwa kasi,ilianza rasmi mwaka 2006, ikiwa na wanafunzi 50, mpaka sasa ina jumla ya wanafunzi 541 wasichana 292 na wavulana 249.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Selema Msumi ( wa kwanza kulia) akikata utepe na familia ya Mkurugenzi wa Kiwanda cha A to Z Textile Mills Limited cha Arusha, Binesh Haria, wakati wakikabidhi darasa hilo kwa shule ya sekondari ya Matevesi.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Selema Msumi ( wa kwanza kushoto) akimkabidhi cheti cha shukurani, ya Mkurugenzi wa Kiwanda cha A to Z Textile Mills Limited Binesh Haria, wakati wakikabidhi darasa hilo kwa shule ya sekondari ya Matevesi
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.