Mkurugenzi wa Arusha DC,Bwana Seleman Msumi amewataka Watumishi wa Umma kuishi maisha ya upendo na kuthaminiana kwani sehemu kubwa ya maishi yao huitumia mahali pakazi.
Ameyasema hayo wakati wa kuwaaga watumishi wastaafu toka Idara ya Elimu katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari ya Ilboru Arusha.
Msumi amesema Watumishi wa Umma wana muda mchache sana wa kukaa na familia zao huku muda mwingi wakiutumia mahali pa kazi hiyvyo kuwataka kuishi kwa upendo na kuchukulia mapungufu na kusameheana kwani kwa kufanya hivyo watakuwa na maisha yenye afya njema ikiwemo afya ya akili.
" Miaka ya hivi karibu Taifa letu limekumbwa na tatizo la watu wengi kukumbwa na msongo wa mawazo unaotokana na aina ya maisha hivyo dawa yake kubwa ni maisha ya upendo"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.