Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, amepongezwa kwa matumizi ya mapato katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, sambamba na usimamizi mzuri wa miradi hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi wakati akizindua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Mateves, utakaojenhwa kwa awamu, ambao umeanza kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje - OPD, mradi uliogharimu shilingi milioni 196 na baadaye kuendelea na majengo mengine ili kuwa na hadhi ya Kituo cha afya.
Amesema kuwa, halmashauri ya Arusha ni miongoni mwa Halmashauri nchini, inayozingatia maelekezo ya Serikali, ikiwemo kutumia mapato ya ndani katika kutekeleza miradi ya maendeleo kulingana na mahitaji ya wananchi wa eneo husika.
"Ninampongeza Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kuzingatia maelekezo ya matumizi ya fedha za mapato ya ndani, kwa kuangalia jengo hili la OPD ni jemgo la kisasa lenye sifa zote za huduma za wagonjwa wa nje, lakini zaidi limejengwa kwa viwango vya ubora vliozingatia thamani ya fedha". Amesema Ussi.
Ameongeza kuwa licha ya kuwa na mradi wa uwezeshaji vijana kiuchumi unaotumia mapato ya ndani lakini wametenga eneo la michezo pia, hivyo ni dhahiri dhamira ya Serikali ya awamu ya sita, inatekelezwa kwa vitendo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.