Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha ndugu Suleman Msumi, amewahimiza wananchi wa makundi yote kuendelea kujitokeza katika sherehe za nane nane zinazofanyika katika viwanja vya Themi-Njiro mkoani Arusha kwa Kanda ya Kaskazini.
Msumi ameyasema hayo alipotembelea mabanda ya Halmashauri hiyo na kueleza kuwa mwaka huu kama Halmashauri wameandaa mambo mazuri zaidi kulinganisha na mwaka jana.
"Nje ya maonesho ya kilimo na ufugaji tuna huduma ya upimaji wa afya, kuna mobile clinic hapa ambapo wananchi wanapata fursa ya kupima afya zao bure, vipo vipimo kama vya VVU na Ukimwi, vipimo vya presha, homa ya Ini pamoja na chanjo hivyo nitumie nafasi hii kuwakaribisha wananchi kujongea katika mabanda yetu ili waweze kupata elimu pamoja na huduma za afya" Amesema.
Maonyesho ya kilimo na sherehe za nane nane za mwaka huu ni ya 30 na yata adhimishwa kitaifa katika Mkoa wa Dodoma ambapo siku ya tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu ndiyo itakuwa siku ya kilele chake.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.