Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Bw. Seleman Msumi, amewataka watendaji wa kata kuhakikisha wanahamasisha wazazi kuchangia chakula cha watoto wao shuleni ili kuboresha mazingira ya ujifunzaji na kuimarisha afya za wanafunzi. Akizungumza katika kikao kilichofanyika tarehe 01 Agosti 2025, Bw. Msumi alisema kuwa lishe bora ni msingi muhimu kwa maendeleo ya kielimu ya mtoto.
Amesisitiza kuwa ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha mtoto anapata mlo shuleni, na kwamba halmashauri haitavumilia uzembe kutoka kwa viongozi wa vijiji na kata katika kufuatilia utekelezaji wa suala hilo. Alieleza kuwa wanafunzi wengi hushindwa kuzingatia masomo kwa sababu ya njaa, jambo linalochangia kushuka kwa ufaulu katika baadhi ya shule.
Katika kuhakikisha uendelevu wa mpango huo, Bw. Msumi ameelekeza kila shule kuwa na bustani ya mboga mboga ili kusaidia kupatikana kwa lishe ya uhakika. Amehimiza ushirikiano kati ya walimu, wazazi na wanafunzi katika kuanzisha na kuendeleza bustani hizo, akisisitiza kuwa hatua hiyo itasaidia pia kuwajengea watoto ujuzi wa kilimo na kujitegemea.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.