Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Seleman Msumi, amewaasa watumishi wa umma kujenga tabia ya kuwahi kazini mapema, kushirikiana kwa karibu, na kuepuka migogoro au kuchongeana kazini, ili kutoa huduma bora kwa wananchi na kuchochea maendeleo.
Msumi alitoa wito huo leo, Jumanne tarehe 19 Agosti 2025, wakati akipokea taarifa ya hali ya ulinzi na usalama wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, iliyowasilishwa na kampuni ya Shima Guard Security.
Mapema leo alfajiri, Mkurugenzi huyo alifika katika geti kuu la kuingilia watumishi na magari, akifuatilia nidhamu ya watumishi kuhusu uwahi kazini na namna kampuni ya ulinzi inavyotekeleza majukumu yake.
Aidha, hatua hiyo ni mwendelezo wa utekelezaji wa maazimio na maagizo aliyoyatoa katika kikao kazi cha watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, kilichofanyika Jumatatu, tarehe 18 Agosti 2025, kwa ajili ya robo ya nne ya mwaka.
"Suala la mtumishi wa umma kuwahi kazini ni la lazima. Mtumishi wa umma anapaswa kuwa mtu wa kufuata utaratibu wa hali ya juu," alisema Msumi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.