Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Ndg. Seleman Msumi, mapema leo asubuhi tarehe 18 Agosti 2025, ameongoza kikao cha utendaji Kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ambapo Mkurugenzi alipata fursa ya kutoa maelekezo na maelewano kwa watumishi, wakiwemo Wakuu wa Divisheni na Vitengo, Timu ya Usimamizi wa Hospitali ya Wilaya pamoja na watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri.
Akizungumza na watumishi hao, Mkurugenzi Msumi alisema lengo la kikao kazi hicho ni kuboresha utendaji kazi na kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi wa Wilaya ya Arusha.
Aidha, aliwataka watumishi wote wa umma katika Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa bidii, kuzingatia maadili ya kazi na kudumisha nidhamu kazini. Alisisitiza kuwa Serikali imewaamini kwa kuwapa dhamana ya kuwahudumia wananchi, hivyo ni wajibu wao kutoa huduma bora, kwa wakati na bila upendeleo.
“Nawashukuru sana watumishi wenzangu kwa ushirikiano mnaonipa katika utendaji wa kazi. Ushirikiano huu umewezesha Wilaya ya Arusha kuendelea kupata mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni,” alisema Ndg. Msumi.
Mwisho wa kikao, Mkurugenzi Mtendaji alihitimisha kwa kusisitiza kuwa utendaji kazi wa Halmashauri lazima uzingatie Mkataba wa Huduma kwa Mteja. Pia alikumbusha umuhimu wa utunzaji wa siri za Serikali, huku akiwataka watumishi kufanya kazi kwa bidii badala ya kuandaa ajali zisizo za lazima kazini. Alisisitiza utoaji wa haki bila upendeleo, umuhimu wa kufika kazini kwa wakati pamoja na kuwepo kwa daftari la mahudhurio na mwongozo wa watumishi wanaotoka nje ya ofisi wakati wa kazi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.