MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMAURI YA WILAYA YA ARUSHA AWATAKA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA WELEDI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Suleman Msumi, @sulleh_msumi ametoa wito kwa watumishi wote wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanatoa huduma kwa weledi na kwa kuzingatia sheria, taratibu, na kanuni zilizowekwa.
Akizungumza katika mkutano na watumishi wa Idara na Vitengo vyote wa Halmashauri uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, Mkurugenzi Msumi amesisitiza umuhimu wa kila mtumishi kuwajibika kutekeleza majukumu yake kwa bidii na weledi.
Msumi amesema kuwa, jukumu la kila mtumishi wa umma ni kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kutumia lugha rafiki na yenye staha kwani kumekuwa na baadhi yetu tunapotoa huduma kutumia lugha zisifaa,hili siyo sawa.
"Ni muhimu kuhakikisha tunapowahudumia wananchi tunatumia lugha rafiki hususan tunapowapa maelekezo juu ya jambo fulani," alisema Msumi.
Aidha, Mkurugenzi Msumi amewakumbusha watumishi wote kuwa na nidhamu ya kazi kwa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kikamilifu katika maeneo yao ya kazi kwa kufuata sheria za Utumishi wa umma.
Sambamba na hilo, amesisitiza umuhimu wa kutunza siri za Serikali na kuhakikisha kuwa kila jambo linazungumziwa kwa uangalifu na mahali husika ili kuzuia uvujaji wa taarifa ambazo hazistahili kuwekwa wazi.
"Ni lazima tuhakikishe tunazingatia maadili ya utumishi wa umma na kuweka kipaumbele kwa masilahi ya wananchi. Hii itaongeza imani yao kwetu kama watumishi wa serikali," Msumi
Mwisho, aliwataka watumishi wote kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila kwa lengo la kuimarisha ufanisi na maendeleo ya Halmashauri hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.