Na. Elinipa Lupembe.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha Saad Mtambule, ameanza rasmi kazi katika halmashauri ya Arusha, kwa kutana na timu ya Menejimenti ya Halmashauri hiyo, mara baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Mheshimiwa Rais, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli mapema mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkurugenzi Mtambule amewataka watumishi hao, kuendelea kufanyakazi kwa bidii, kwa kufuata miongozo, kanuni, taratibu na sheria za utumishi wa Umma, huku nguvu kubwa ikielekezwa kufanyakazi kama timu, lengo likiwa ni kuwatumika wananchi wa halmashauri ya Arusha.
"Halmashauri ni taasisi yenye watalamu wa kada tofauti na kazi zake hufanyika kwa kutegemeana, hivyo tukifanya kazi kama timu tutafanikiwa kufikia malengo ya halmashauri na Serikali kwa ujumla"
Hata hivyo, timu hiyo ya Menejimenti, imamkaribisha mkurugenzi huyo mgeni na kuahidi kumpa ushirikiano wa hali na mali katika kutekeleza majukumu yake, kama ilivyokuwa kwa wakurugenzi waliotangulia, katika halmashauri hiyo, lengo likiwa ni kutoa huduma bora kwa wananchi kwa maendeleo endelevu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.