Na Elnipa Lupembe
Mkuu wa shule ya Sekondari Ilkiding'a, halmashauri ya Arusha m Mwl. Supeet Sailevu na familia yake, tayari ametimiza wajibu wake kwa Serikali, kama Mkuu wa Kaya, kwa kuhesabiwa kwenye Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake eneo Olosiva kata ya Oloirieni mapema leo.
Mkuu huyo wa shule ameataka wananchi ambao hawajahesabiwa kuwa wavumilivu kwa kuwa Makarani wa Sensa watafika kwenye kaya zao, kinacgohitajika ni kuwapa ushirikiano na kutoa taarifa zote zilizoandaliwa wkenye dodoso la Sensa.
"Niwatoe hofu watanzania wenzangu, licha ya kuwa dododso lina maswali mengi, lakini naweza kusema ni maswali yanayoulizwa ni maswali yanayojibika na yako ndani ya uwezo wetu, hivyo tuhakikishe tumehesabiwa kwa mipango bora ya Serikali yetu kwa maendeleo ya Taifa letu". Amesisitiza Mwl. Supeet
HAKIKISHA UMEHESABIWA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.