Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh. Mwinyi Ahmed Mwinyi siku ya tarehe 09/07/2025 amefanya kikao kazi na viongozi wa Halmashauri pamoja na wa taasisi za serikali zilizopo katika Wilaya ya Arusha DC.
Mh.Mwinyi Ahmed Mwinyi alisema lengo kuu la kikao hiki ni kujitambulisha kwenu nikiwa ndiye Mkuu wa Wilaya hii baada ya mabadiliko yaliyofanywa na Mh. Rais siku chache zilizopita, na pia kuwatambua nyie viongozi wote mliopo mahali hapa, pamoja na kuomba ushirikiano wenu ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano katika kuhakikisha tunawaletea wananchi wa Wilaya hii maendeleo na kuhakikisha wanaishi kwa amani, furaha na usalama.
Katika kikao hicho viongozi kutoka ngazi ya vijiji, kata na wote walihudhuria, ambapo walimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwaalika katika kikao hicho na kumuahidi kumpa ushirikiano wote katika kuhakikisha wanawaletea maendeleo wananchi wa Wilaya ya Arumeru katika katika sekta zote za elimu, Afya, maji, nishati na miundombinu iliyo bora na mizuri.
Mkuu wa Wilaya aliwaomba Viongozi hao kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja na kuhakikisha Kila mtu anatimiza majukumu yake ya Kazi kwa kufuata kanuni, taratibu na Sheria za kazi, na pale wanapohitaji kuonana nae milango ya ofisi yake Ipo wazi na Kila mtu anaruhusiwa kuja kuongea nae pale anapohitaji ufafanuzi au ushirikishwaji wake kama Mkuu wa Wilaya.
Aidha, Mh. Mwinyi alimwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara na Vitengo kuhakikisha wanaandaa Miradi ambayo itatembelewa na mwenge wa uhuru, 2026 wakishirikiana na taasisi katika kuhakikisha maandalizi ya mapokezi ya mwenge yanaanza mapema kwa kubainisha miradi yote na njia ambazo mwenge utapita.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.