Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda amewaelekeza Wataalam wa Kilimo na Ushirika toka Halmashauri ya Arusha kwenda kwa wananchi Kata zote kushughulikia kilio cha Wakulima kuhusu kulazimishwa na Wafanyabiashara kuuza mazao yao kwa ujazo zaidi ya ujazo wa kawaida( lumbesa).
Ameyazungumza hayo wakati akijibu hoja katika Mkutano wa hadhara wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Ndugu. Thomas Ole Sabaya katika kata ya Oltroto Halmashauri ya Arusha.
Miongoni mwa changamoto zilizotajwa ni pamoja changamoto lumbesa kwa wakulima, na maombi ya kituo cha polisi katika Kata hiyo.
Suala la lumbesa Mhe. Kaganda amewataka Maafisa Kilimo na Ushirika kulisimamia kwa kushirikiana na wakulima kwa kuhakikisha kipimo halisi cha kufungia mizigo kinatumika ili pande zote zinufaike.
Mhe. Kaganda amewataka wananchi kushikamana na Serikali katika kutekeleza miradi kama ujenzi wa kituo cha polisi kwani kupitia wadau na wananchi jambo hilo linawezekana kabla ya kusubiria kutoka kwa Serikali.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.