Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Mhe.Emmanuela Mtatifikolo Kaganda amewataka wananchi Wilayani Arumeru kufuata taratibu za kisheria wanapokuwa na hoja dhidi ya Viongozi wao waliowachagua.
Ameyazungumza hayo wakati akiongoea na wananchi wa Kata ya ya Oltrotu katika mkutano wa hadhara ambapo ajenda kuu ilikuwa changamoto ya kuharibiwa miundombinu ya maji iliyofanywa na baadhi ya wananchi wa kata kwa madai ya kuukataa Uongozi wa Kijiji hicho.
Mhe.Kaganda amesema Serikali haiko tayari kuona baadhi ya watu wakichukua sheria mkononi za kuharibu miundombinu iliyojengwa kwa gharama kubwa kwa kisingizio cha kuwa Uongozi haifai kuwaongoza kwasababu zao binafsi zisizokuwa na mashiko kwa Umma.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.