Katika kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yaliyofanyika katika Viwanja vya Themi Njiro, Arusha, Leo Tarehe 08 Agosti 2025, Bw. Mosses Givas Mollel ameibuka mshindi wa tuzo ya Mkulima Bora wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha. Ushindi huo umetokana na juhudi zake katika kutumia mbinu bora za kilimo na kuongeza tija kwa mazao anayolima.
Bw. Mollel alikaidhiwa zawadi ya hundi yenye thamani ya shilingi 600,000/= pamoja na cheti cha kutambua mchango wake katika maendeleo ya sekta ya kilimo. Tuzo hiyo inalenga kuhamasisha wakulima wengine kuiga mfano wake katika kuongeza ubunifu na uzalishaji.
Zawadi hizo zilikabidhiwa na mgeni rasmi wa maadhimisho hayo, Mhe. Nurdin Hassan Babu, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, ambaye alisifu jitihada za Bw. Mollel na kuwataka wakulima kote nchini kuendelea kushirikiana na wataalamu wa kilimo ili kuongeza tija na kuinua kipato cha kaya.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.