Na Elinipa Lupembe
Hatimaye Shule ya sekondari Mringa, imekamilisha ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa, mradi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 80 fedha kutoka Serikali Kuu, maarufu kama 'POCHI LA MAMA', ikiwa ni maandalizi ya kupokea wananfunzi wa kidato cha kwanza, watakaopangiwa kwa mwaka wa masomo utakaoanza Januari 2023.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mkuu wa shule hiyo, Mwl. Salum Magaka ameweka wazi kuwa, shilingi milioni 80 zimetumika kujenga vyumba vinne vya madarasa meza na viti 160.
Aidha Mwl. Magaka, ameitaja siri ya kukamilisha mradi kwa haraka ni hali uhitaji wa madarasa hayo manne, ari ya kazi na kujituma lakini zaidi matumizi ya force akaunt yanayoruhusu ushirikishwaji wa jamii katika kutekeleza.
"Tunamshukuru sana mheshimiwa Rais, shule ilikuwa na uhitaji wa vyumba vinne vya madarasa, na serikali ikaleta fedha za idadi inayolingana na ya uhitaji, uwepo wa madarasa ya kutosha unarahisisha tendo la kujifunza na kufundisha kwa wanafunzi na walimu, mazingira bora huwafanya wanafunzi kupenda shule". Amesema Mkuu huyo wa shule
Awali shule ya sekondari Mringa ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa kwa kidato cha nne na cha sita ina jumla ya wanafunzii 1, 754 huku wanafunzi 1, 379 wa kidato cha kwanza mpaka cha nne, na wawanafunzi 375 wa kitado cha tano na sita.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
MUONEKANO WA VYUMBA VYA MADARASA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.