Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule amemkabidhi rasmi, fomu za Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi Bi. Arafa Mohamed Muya kupitia Chama cha Wananchi CUF.
Mgombe huyo wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF, amekabidhiwa fomu hizo, mnamo saa 04:20 asubuhi ya leo, kwenye Ofisi ya Msimamizi Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Ofisi iliyopo kwenye Ofisi za Makao Makuu Halmashauri ya Arusha eneo la Sekei.
Aidha Msimamizi huyo wa Uchaguzi, amemkabidhi fomu ya Uteuzi mgombea huyo, kufuatia Maelekezo ya Fomu ya Uteuzi Na. 8B, kwa mujibu wa Kifungu cha 38 (3) na (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 ikiweka wazi mambo yaliyojumuishwa kwenye fomu ya Uteuzi.
Bi. Arafa Mohamed kupitia Chama cha Wananchi CUF, amekuwa Mgombea wa kwanza kuchukua fomu ya Uteuzi wa Ubunge kwa Jimbo la Arumeru Magharibi.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule (kulia) akimkabidhi fomu ya Uteuzi wa Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi Bi. Arafa Mohamed Muya kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo hilo mnamo saa 04:20 asubuhi ya leo.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF, Bi Arafa Mohamed Muya, akisaini kitabu cha kukiri kupokea fomu ya Uteuzi kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF, Bi Arafa Mohamed Muya, akisaini kitabu cha kukiri kupokea fomu ya Uteuzi mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF, Bi Arafa Mohamed Muya, akihakiki fomu ya Uteuzi kabla ya kusaini kukiri kuipokea kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.