Na. Elinipa Lupembe.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Halmashauri ya Arusha, mwalimu Hosein Mghewa, ametangaza rasmi, majina ya Mipaka ya vijiji iliyoko katika eneo la halmashauri ya Arusha, kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kijiji cha Marurani, kata ya Nduruma, Halmashauri ya Arusha.
Akitangaza Mipaka hiyo, Mghewa amesema kuwa, "Kwa Mamlaka niliyopewa chini ya Kanuni ya 5 ya Kanuni ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Mji Mdogo Tangazo la Serikali namba 371 la tarehe 26.04.2019 pamoja na Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya, Tangazo la Serikali namba 373 la tarehe 26.04.2019 na kwa kuzingatia Orodha ya Vijiji na Vitongoji vilivyotangazwa katika Gazeti la Serikali Namba 537 la tarehe 19.07.2019".
Msimamizi huyo wa Uchaguzi ametangaza majina ya mipaka halmashauri ya Arusha kuwa jumla ya Vijiji 67 na Vitongoji 259.
Tangazo hilo ni mchakato kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa, unaotegemea kufanyika tarehe 24.11.2019.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.