Na. Elinipa Lupembe.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule amekabidhi tena, fomu za Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi wateule wawili, Bi. Farida Marko Nnko kupitia Chama cha UMD na Bi. Tumaini Andrea Akyoo wa Chama UPDO.
Wagombea wote wawili wa vyama tofauti waliwasili kwa pamoja, kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi eneo la Sekei majira ya saa 08:10 mchana na kukabidhiwa fomu hizo za Uteuzi kwania nafadi ya Mbunge wa Jimbo hilo.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo, alimkabidhi fomu za uteuzi wa nafasi ya Ubunge Bi. Frida Marko Nnko kupitia Chama cha UMD mnamo saa 08:26 mchana, huku Bi. Tumaini Andrea Akyoo, alikabidhiwa fomu hizo majira ya saa 08:27 mchana.
Aidha Msimamizi huyo wa Uchaguzi, amewakabidhi fomu ya Uteuzi mgombea huyo, kufuatia Maelekezo ya Fomu ya Uteuzi Na. 8B, kwa mujibu wa Kifungu cha 38 (3) na (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 ikiweka wazi mambo yaliyojumuishwa kwenye fomu ya Uteuzi.
kwenye fomu ya Uteuzi.
Hata hivyo Mutambule, mewataka wateule hao, kutumia muda kusoma melekezo yaliyotolelewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kupitia vitini walivyokabidhiwa, ikiwa ni pamoja na kutumia lugha zenye staha wakati wa Kampeni na kuepuka maneno ya kashfa kwa wagombea wengine, kuwaelimisha wafuasi wa vyama vyao kuwa watulivu ili uchaguzi uwe wa amani, huru na wa haki
Wagombea hao wawili wamefanya kufikisha idadi ya Wagombe watatu kutoka vyama vitatu vya siasa, kuchukua fomu za Uteuzi wa Ubunge kwa Jimbo la Arumeru Magharibi.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule (kulia), akimkabidhi fomu ya Uteuzi wa Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi Bi. Tumaini Andrea Akyoo kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha UPDP.
Bi. Tumaini Andrea Akyoo akisani daftari la kukiri kupokea fomu ya Uteuzi wa Ubunge kupitia Chama cha UPDP, mara baada ya kukabidhiwa fomu ya Uteuzi wa Ubunge na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule (kulia), akimkabidhi fomu ya Uteuzi wa Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi Bi. Frida Marko Nnko kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha UMD.
Bi. Frida Marko Nnko akisani daftari la kukiri kupokea fomu ya Uteuzi wa Ubunge kupitia Chama cha UMD mara baada ya kukabidhiwa fomu ya Uteuzi wa Ubunge na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.