Na. Elinipa Lupembe.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule amemkabidhi fomu za Uteuzi wa Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi, Bw. Gibson Ole Meseiyeki, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA.
Mgombea huyo aliwasili kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo, eneo la Sekei akiwa ameambatana na wafuasi wa chama hicho, majira ya saa 03:10 asubuhi, na kukabidhiwa fomu hizo za Uteuzi majira ya saa 03:52 asubuhi kwa kuwania nafasi ya Mbunge wa Jimbo hilo.
Aidha Msimamizi huyo wa Uchaguzi, amemkabidhi fomu ya Uteuzi mgombea huyo, kufuatia Maelekezo ya Fomu ya Uteuzi Na. 8B, kwa mujibu wa Kifungu cha 38 (3) na (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 ikiweka wazi mambo yaliyojumuishwa kwenye fomu ya Uteuzi.
Hata hivyo Mtambule, amemtaka mteule huyo, kusoma melekezo yaliyotolelewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kupitia vitini vya maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, sambamba na kuheshimu taratibu za uchaguzi kwa kuepuka maneno ya kashfa kwa wagombea wengine wakati wote wa Kampeni, huku wakiwaelimisha wafuasi wa Chama chao kuwa watulivu na wastahimilivu kwa lengo la kufanya uchaguzi kuwa wa amani, huru na haki.
Mgombea huyo amefanya kufikisha idadi ya Wagombe sita kutoka vyama sita vya siasa, kuchukua fomu ya Uteuzi wa Ubunge kwa Jimbo la Arumeru Magharibi.
PICHA ZA MATUKIO
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule (kulia), akimkabidhi fomu ya Uteuzi wa Ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi Bw. Gibson Ole Meseiyeki, kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA.
Bw. Gibson Ole Meseiyeki akisani daftari la kukiri kupokea fomu ya Uteuzi wa Ubunge kupitia Chama cha UPDP, mara baada ya kukabidhiwa fomu ya Uteuzi wa Ubunge na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.