MSUMI AELEKEZA MBINU ZA USHINDI
Katika kuelekea michuano ya SHIMISEMITA itakayofanyika jijini Tanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Bw. Seleman H. Msumi, leo tarehe 15 Agosti 2025, ameipatia timu ya halmashauri hiyo mbinu mahsusi za kufanikisha ushindi.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wachezaji hao, Bw. Msumi alisisitiza kuwa mbinu ya kwanza na ya msingi ni kudumisha nidhamu wakati wote wa mashindano. Aidha, aliwataka wachezaji kujituma, kuhamasishana, na kusikiliza kwa makini maelekezo ya walimu wao (coaches) ili kuimarisha uimara wa timu na kuongeza nafasi ya ushindi.
“Timu yenye nidhamu, mshikamano na utii wa maelekezo ndiyo inayoweza kushinda. Nawaamini mnaweza,” alihitimisha Bw. Msumii.
Mbali na hayo, aliwatakia safari njema kuelekea Tanga na kuwataka wasisite kutoa taarifa mara tu changamoto yoyote inapojitokeza wakiwa safarini au wakiwa kwenye mashindano.
KAULIMBIU " Jitokeze kupiga kura Katika uchaguzi Mkuu kwa Maendeleo ya Michezo"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.