Na. Elinipa Lupembe.
Muasisi wa Mradi wa maji wa Vijiji Vitano na Diwani wa kata za Enderbay na St. Johns, nchini Uingereza, Bi. Louise Richardson na mkurugenzi wa shirika la Tumain Jipya- New Hope, ameungana na watanzania kushuhudia, mradi huo, ukiwekwa Jiwe la Msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali.
Bi. Louise ndiye muasisi wa mradi huo mkubwa wa maji,baada ya kuishi kwa muda katika kijiji cha Lengijave na kushuhudia adha kubwa ya maji waliyoipa wananchi wa maeneo hayo, na kuguswa hasa na wanafunzi wa kike walioshindwa kupata maji walau ya kujisitiri wawapo kwenye siku zao.
Louise aliporejea nchini kwake, aliwasilisha hitaji hilo la wananchi wa Lengijave, kwwenye Serikali ya Uingereza, kupitia bunge la Serikali hiyo na kuamua kusaidia ujenzi na upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Lengijave na vijiji vingine vinne.
Mradi wa maji wa vijiji vitano unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 8.4, kwa ufadhiliwa na Idara ya Maendeleo Uingereza 'DFID', unategemea kuhudumia watu elfu 50 wa vijiji vya Lengijave na Olkokola na Vitongoji vya Ekenywa, Seuri na Olmotony vya Mamlaka ya Mji mdogo Ngaramtoni.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro na Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera kwa pamoja wanatoa shukrani za dhati kwa Mama Louise kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Dkt. John Magufuli, na kuhakikisha kila mwananchi anachota maji ndano ya mita 400.
Mradi huu umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake na unategemea kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu 2019, aidha, kukamilika kwa mradi huu, halmashauri ya Arusha, itafikisha asilimia 75 ya idadi ya wananchi wanaopata maji safi na salama.
Kongole kwake Mama Louise Richardson.
#PamojatunajengaTanzania#
Jiwe la msingi lililowekwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019, ndugu Mzee Mkongea Ali, kwenye mradi wa maji wa vijiji vitano.
Timu ya wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019, ikiongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019, ndugu Mzee Mkongea Ali, kukagua moja ya tanki la kuhifadhia maji kwenye mradi wa maji wa vijiji vitano, na kujiridhisha, kabla ya kuweka jiwe la msingi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019, ndugu Mzee Mkongea Ali, akikagua moja tanki la kuhifadhia maji kwenye mradi wa maji wa vijiji vitano, na kujiridhisha kabla ya kuweka jiwe la msingi.
Mwenge wa Uhuru 2019 ukiwasili eneo la shamba la mbegu ASa, mahali kwenye vyanzo viwili vya maji, nyumba za kusukuma maji, matanki ya kuhifadhia maji pamoja na nyumba ya kuchuja na kuchakata maji.
Picha ya pamoja Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro na Timu ya Tumaini Jipya (waliovaa flana nyeupe) wakiongozwa na Mama Louise Richardson wa (wa nne kutokakushoto), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha mhe. Noah Lembris wa tatu kutoka kulia, Diwani wa Kata ya Lengijave mhe. Kalanga Laiza wa pili kushoto.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.