Huu ndio muonekano mpya wa Kituo cha Afya Nduruma mara baada ya zoezi la upanuzi na ujenzi wa miundombinu ya kituo hicho kukamilika kwa zaidi ya asilimia 95% kuelekea kuanza kutumika kwa majeno mapya kwa kutoa huduma kwa wagonjwa.
Ujenzi wa miundombinu hiyo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 500 fedha zilizotolewa na serikali, mwishoni mwa mwaka 2017, kufuatia adhma ya serikali ya awamu ya tano ya kuboresha miundombinu kwenye vituo vya afya na hospitali.
Aidha kiasi hicho cha fedha, kimetumika kujenga majengo mapya katika kituo hicho ikiwemo maabara, jengo la upasuaji, wodi ya mama na mtoto ' martenity ward' jengo la kujifadhia maiti, kichomea taka, vibaraza 'walk ways', nyumba ya mganga pamoja na umaliziaji wa jengo la Kliniki ya mama na mtoti na ushauri nasaha 'CTC'.
Kwa kipindi kifupi serikali ya awamu ya tano, imeweza kuongeza bajeti ya dawa kutoka bilioni 31 mpaka bilioni 269 ili kuhakikisha dawa zinapatikana pamoja na kukarabati vituo vya afya 205 ikiwemo kituo cha afya Nduruma.
Upanuzi na uboreshaji wa vituo vya afya unategemewa kutoa matibabu muhimu kwa wananchi katika maeneo wanayoishi, pamoja na kutoa huduma za uzazi kwa kina mama wajawazoto na kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.