*MWAROBAINI WAANDALIWA KWA WATOA HUDUMA ZA FEDHA WAKAIDI*
Watoa huduma za Fedha Nchini wametakiwa kufuata Sheria na taratibu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ikiwemo kujisajili, kutoza viwango sahihi vya riba na kuwapa nakala za mikataba wakopaji ili kuepuka adhabu kwa wanaokiuka Sheria za huduma za fedha.
Akitoa elimu ya fedha kwa wajasiliamali na wananchi wa Kata ya Ilikiding’a Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw Salim Kimaro amewataka wajasiliamali hao kusajili vikundi vyao vya huduma ndogo za fedha ili kulinda fedha zao dhidi ya wanakikundi wasiyo waaminifu.
‘’Hatusemi vile vikundi vyenu ambavyo havijasajiliwa mvivunje hapana, ni vizuri ila nendeni mkavisajili, kama wale mliowaona kwenye filamu wangesajili kikundi chao na kuweka hela benki fedha zao zisingepotea’’ alisema Bw. Kimaro.
Naye Afisa Mwandamizi, Uchambuzi Fedha, Idara ya Sera, Utafiti na Mipango, kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA. Gladness Mollel, amewashauri wajasiliamali hao kuwekeza katika njia mbalimbali ikiwemo zile walizofundihswa na watalam wa elimu ya fedha kwa ajili ya kujikimu katika kila hali ya maisha.
‘’Kuna njia nyingi za uwekezaji ikiwemo hatifungani kuna aina mbalimbali za hatifungani, kwanza zipo hatifungani za Serikali na pia zipo hatifungani za kampuni na taasisi nyingine’’ alisema Bi. Gladness.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Bw. Seleman Msumi, amewahakikishia wataalamu hao wà usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha toka Wizara ya Fedha kuwa ofisi yake itatoa ushirikiano kwa kutoa elimu zaidi Ili vikundi ndani ya Halmashauri hiyo vinavyotoa huduma za kifedha katika masuala ya ujasilimali kujisajili ilikukidhi matakwa ya kisheria wanapotoa huduma kwa wanachama wao.
Aidha, Lulu Mesikana ambaye ni mmoja wa wajasiliamali waliohudhuria mafunzo hayo ya elimu ya fedha, aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu hiyo kwa wananchi huku akiomba programu hiyo ya elimu ya fedha iwe endeevu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.