Na Elinipa Lupembe
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Sahil Nyanzabara Geraruma, amezindua ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa shule ya sekondari Oldadai, Mradi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 40 Fedha za mapambano dhidi ya UVIKO-19
Katika shule hiyo ya sekondari Oldadai, Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, amekagua mradi wa ukamilishaji ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa, mradi uliogharimu shilingi milioni 40.5 ikiwa ni michango ya wananchi gedha za tozo ya miamala ya simu pamoja na kuzindua Klabu ya TAKUSKA ikiwa ni muunganiko wa Klabu ya Wapinga Rusha na Skauti.
Aidha amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii kwa kuwa serikali imetumia pesa nyingi kujenga miundo mbinu ya shule lengo likiwa ni kuhakikisha watoto wa kitanzania wanasoma katika mazingira maauri na kuweza kufaulu vizuri masomo yao.
Kauli Mbiu:
SENSA NI MSIMGI WA MIPANGO YA MAENDELEO: SHIRIKI KUHESABIWA, TUYAFIKIE MAENDELEO.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.