DC ARUMERU APOKEA MWENGE WA UHURU 2023
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, amepokea Mwenge wa Uhuru 2023,kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Longido Mhe. Marco Ng'umbi kwenye eneo la Soko la Oldonyosamba, tayari kwa kukimbizwa kwenye halmashauri mbili za Arusha na Meru za wilaya hiyo.
Mhe. Emmanuela amesema kuwa, katika wilaya ya Arumeru, Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023, zitakimbizwa umbali wa Kilomita 204.3 kwenya halmashauri mbili za Arusha na halmashauri ya Meru Meru na kukagua jumlanya miradi 16 yenye thamani ya shilingi Bilioni
Aidha , Mwenge wa Uhuru ukiwa katika halmashauri ya Arusha, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu Abdalla Shahib Shakim ataukimbizwa umbali wa Km 88.4 na kukagua miradi 8 yenye thamani ya shilingi bilioni 8.5 katika sekta ya maji, elimu, afya, miundombinu ya barabara pamoja, vikundi vya wajasiriamali, uwekezaji na utunzaji wa mazingira hususani kwenye vyanzo vya maji.
Ameongeza kuwa, Mwenge wa Uhuru ukiwa katika halmashauri ya Meru, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu Abdalla Shahib Shakim ataukimbizwa umbali wa Km 115.9 na kukagua miradi 8 yenye thamani ya shilingi bilioni 8.7 katika sekta ya maji, elimu, afya, miundombinu ya barabara pamoja na vikundi vya wajasiriamali.
KAULI MBIU: " TUNZA MAZINGIRA, OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI WA VIUMBE HAI KWA UCHUMI WA TAIFA"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.