Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha ndg.Thomas Ole Sabaya amewataka viongozi wa chama na Serikali ngazi ya vijiji na Kata kujenga utamaduni wa kuitisha mikutano ya hadhara ya mara kwa mara ili kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi changamoto za wananchi.
Sabaya ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Kata ya Oltroto Halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru.
"Itaneni mara kwa mara ili kujenga uelewa wa pamoja katika kuzishughulikia changamoto mlizonazo na itawafanya mjenge uhusiano mzuri na wale mnaowaongoza" Amesema.
Naye mkuu wa Wilaya Mh. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda amewataka wananchi wanaoshughulika na kilimo kutokubali kurubuniwa na kuuza mazao yao kwa mtindo wa Lumbesa, kitendo kinachowafanya wakulima hao kupata hasara.
Ameyaeleza hayo kutokana na malalamiko ya baadhi ya wakulima Katani hapo ambao wamedai juu ya wanunuzi wanaoendelea kukaidi maagizo ya Serikali kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika maeneo mengine.
"Niwaombe ndugu zangu wakulima, pamoja na kwamba Serikali itachukua hatua, lakini hatua ya kwanza ni juu yenu kuwa wamoja, mkiweka msimamo kuwa hamtauza kwa mtindo wa Lumbesa hao wanunuzi hawatashuka na magunia yaliyo wazi watanunua tu"
Ziara ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha katika Halmashauri ya Arusha, inalenga katika kusikiliza na kutatua kero za wananchi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza, wakati utakapofika wa kujiandikisha katika daftari la kudumu ili waweze kushiriki vema katika chaguzi zijazo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.