Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Arusha Ndg. Thomas Loy Ole Sabaya amefanya kikao cha hadhara katika Kata ya Kiranyi Halmashauri ya Arusha tarehe 2 Agosti 2024.
Ndg. Ole Sabaya amewahimiza viongozi wa mitaa, vijiji kuhamasisha wananchi kujitokeza na kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la Wapiga kura.
Pia amewahimiza wananchi kuchagua viongozi sahihi wanaofaa kuwaongoza na si wazururaji.
“Usichague kiongozi kwasababu ya ukoo, Kabila au mwenye maneno mengi bila matokeo, bali chagueni viongozi wanaofaa, wanaowajibika na kutatua changamoto za wananchi” amesema.
Aidha, ameongeza kuwa viongozi wanatakiwa kusimamia miradi na kuhakikisha inamalizika kwa muda uliopangwa.
Ziara hii ya Kichama ni mwendelezo wa ziara za Mwenyekiti huyo kupita kila Kata katika Mkoa wa Arusha kwa lengo la kusikiliza kero za Wananchi Vijijini na kuzitafutia ufumbuzi huku akiwa ameongozana na Mbunge wa Arumeru Magharibi,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha Mkurugenzi akiwa na Wataalam wa Halmashauri ya Arusha pamoja na Taasisi nyinginezo za Umma.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.