Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (Rufaa) Jacob Mwambegele akizungumza na Maafisa waandikishaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika Halmashauri ya Arusha mara baada ya kukamilika kwa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa BVR yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano shule ya Sekondari ya Ilboru.
Mkoa wa Arusha unatarajia kuanza rasmi zoezi uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kuanzia tarehe 11 -17 mwezi disemba 2024 katika Halmashauri zake zote.
Kwa Halmashauri ya Arusha zoezi hilo linatarajiwa kufanyika katika Kata zote 27 ambapo Vituo vya uandikishaji vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni
Zoezi hilo la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa mwaka 2024 limebeba kauli mbiu inayosema "Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.