• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

NAIBU WAZIRI NDEJEMBI AIAGIZA TASAF KUTEKELEZA UJENZI WA UZIO SHULE YA SEKONDARI OLDONYOWAS

Posted on: July 14th, 2022

Na Elinipa Lupembe

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deogratius John Ndejembi ameuagiza uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kutekeleza ujenzi wa uzio katika shule ya sekondari Oldonyowas ili kulinda Miundombinu ya madarasa na mabweni iliyojengwa katika shule, ikiwa ni pamoja na usalama wa wanafunzi wa shule hiyo.

Naibu Waziri Ndejembi amesema hayo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa ujenzi wa mabweni mawili ya wavulana katika shule hiyo, Mradi unaotekelezwa na TASAF III awamu ya II kwa ufadhili wa  OPEC International Fund, na kuweka wazi kuwa, kukamilika kwa miundombinu ya shule hiyo, uende sambamba na ujenzi wa uzio wa shule hiyo ili kuhakikisha usalama wa shule na wanafaunzi.

“Nimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi huu wa mabweni kutokana na ushirikishwaji wa wananchi wa eneo hili, kwa kuwapa ajira za muda na kujipatia kipato kama ilivyo mpango wa TASAF wa kuzikomboa kaya zenye kipato cha chini, niwatake TASAF kuweka mkakati wa kujenga uzio katika shule hii kwa ajili ya usalama wa mali na wanafunzi”. Amesema Mhe. Ndejembi

Naye Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Mhe. Noah Lembris amesema kuwa uwepo wa mabweni hayo utasaidia utulivu kwa wanafunzi hasa wale wanaotembea umbali mrefu kwenda na kurudi shuleni kuondokana na adha hiyo, hali itakayochangia kupanda kwa taaluma na ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi shuleni hapo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango, licha ya kuishukuru serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni hayo, amewataka viongozi pamoja na wananchi kila mtu kutekeleza wajibu wake kama kanuni na taratibu za serikali zinavyoelekeza ikiwemo kutunza na kulinda miradi yote inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao.

Awali akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,  Oscar Maduhu, amesema kuwa lengo la miradi hiyo ni kuondoa adha iliyopo katika maeneo yenye uhaba wa miundombinu katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu na afya, lengo likiwa ni kupambana na adui maradhi, ujinga na umasikini.

“TASAF itaendelea kutekeleza miradi mingine kwa ajili ya kuwahudumia wananchi kisekta, niwatake wananchi kuendelea kujitoa katika kutekeleza miradi pamoja na kuhakikisha miradi hiyo, inakamilika kwa viwango vinavyokubalika, ili kufikia lengo la serikali la kuwahudumia wananchi wa kipato cha chini,  zaidi niwatake kuitunza miradi hiyo ili idumu kwa muda mrefu na kuhudumia wanafunzi wetu”. Amesisitiza Maduhu.

Elieshi Gabriel ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Oldonyowas ameweka wazi kuwa, Watoto wao walikuwa wanatembea umbali mrefu sana wakivuka makorongo makubwa kufika shuleni hapo, na wakifika nyumbani wanakuwa wamechoka sana kiasi cha kutoweza kujisomea wenyewe hivyo uwepo wa mabweni hayo utasadia Watoto wao kuwa salama na ufaulu wao kuongezeka. 

Mradi huo wa ujenzi wa mbweni mawili ya wavulana umetekelezwa kwa gharama ya Zaidi ya shilingi milioni 300 baada ya kukamilika kwa mabweni ya wasichana katika shule hiyo na yanatarajiwa kubeba jumla ya wanafunzi 160.

ARUSHA DC

KaziInaendelea 

JIANDAE KUHESABIWA.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deogratius John Ndejembi, akikagua mradi wa ujenzi wa Mabweni ya wavulana shule ya sekondari Oldonyowas, mradi unaotekelzwa na TASAF kwa gharama ya shilingi milioni 300.






Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deogratius John Ndejembi, akikagua mradi wa ujenzi wa Mabweni ya wavulana shule ya sekondari Oldonyowas, mradi unaotekelzwa na TASAF kwa gharama ya shilingi milioni 160.















Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.