• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

NAIBU WAZIRI MKUU DKT DOTTO BITEKO ATOA RAI YA KUDUMISHA TUNU YA MUUNGANO - ARUSHA

Posted on: April 25th, 2025


NAIBU WAZIRI MKUU DKT DOTTO BITEKO ATOA RAI YA KUDUMISHA TUNU YA MUUNGANO - ARUSHA



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, amewasihi Watanzania kuenzi na kudumisha tunu ya Muungano ulioasisiwa na waasisi wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, akisisitiza kuwa amani na mshikamano wa Taifa ni nguzo muhimu ya maendeleo.



Akizungumza Leo  katika mkutano wa hadhara wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Dk. Biteko alieleza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha maendeleo yanamfikia kila Mtanzania, huku akibainisha kuwa zaidi ya shilingi bilioni 100 zimetolewa kwa halmashauri za Arusha na Meru kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.


“Halmashauri ya Arusha imepokea shilingi bilioni 49 na Meru zaidi ya bilioni 52. Haya ni maendeleo yanayoonekana kwa macho. Tunapaswa kuilinda amani yetu kwa gharama yoyote, kwani Tanzania ni nchi pekee ambako watu wa dini zote na wasiokuwa na dini wanaishi kwa mshikamano,” alisema Dk. Biteko.



“Wapo wanaosema tupigane kidogo. Hii si hoja. Amani inalindwa kwa gharama kubwa. Tusiichezee,” alisisitiza.


Kuhusu miundombinu, Naibu Waziri Mkuu alieleza kuwa serikali inatarajia kupanua barabara ya Arusha–Tengeru kuwa ya njia nne ili kupunguza msongamano na kuchochea maendeleo ya kiuchumi. Alisema serikali inaendelea kuwekeza kwenye sekta muhimu kama nishati, elimu na afya, ili kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.



“Tanzania sasa inatimka vumbi kwa miradi ya maendeleo. Serikali inasikiliza na kutatua kero za wananchi. Hii ni dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo.”



Katika ziara hiyo, Dk. Biteko aliweka jiwe la msingi kwenye jengo la utawala la Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 5.664. Mradi huo unatekelezwa chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, ukitarajiwa kukamilika Mei 17, 2025.



Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo cha TCDI, Dk. Bakari George, hadi sasa ujenzi huo umeshagharimu shilingi bilioni 2.7. Jengo hilo litakuwa na ghorofa tatu, sakafu nne, ofisi 44 na kumbi tano zitakazochukua watu 545 kwa wakati mmoja. @arusha_district_council  @amir_mkalipa  @sulleh_msumi


Matangazo

  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA TATU 2O21/2022 tarehe 09.05.2022 May 08, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA ARUSHA DC,BW.SELEMAN MSUMI AKIWA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI HIYO KATIKA MASDHIMISHO YA MEI MOSI KIMKOA ARUSHA

    May 02, 2025
  • HERI YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • HERI YA SIKU YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • MHE. MAJALIWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.