• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara ameahidi kushughulikia tatizo la maji na barabara Sekondari Mwandet

Posted on: April 28th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais -TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Elimu Mheshimiwa, Mwita Waitara, ameahidi kushughulika changamoto ya maji na miundombinu ya barabara, zinazoikabili shule ya sekondari Mwandet, halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru.

Naibu Waziri, Waitara ametoa hadi hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea shule za sekondari Mwandeti na Mlangarini katika halmashauri hiyo, kwa lengo la kukagua miradi inayotekelezwa na Serikali, kupitia fedha za miradi ya Lipa kutokana na Matokeo 'EP4R', na kupata wasaa wa kuzungumza na wanafunzi, viongozi wa kata na bodi za shule hizo.

Ahadi hiyo imekuja, mara baada ya wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Mwandet, kutoa kilio chao, cha uhaba wa maji shuleni hapo, ubovu wa barabara ya kuingia shuleni pamoja na upungufu wa nyumba za walimu, changamoto wanazodai wakati mwingine, zinawapotezea muda wa kujikita kwenye masomo.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Dada Mkuu wa shule hiyo, Riziki Joseph, amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa, katika eneo la shule yao hakuna maji, jambo linalowalazimu wanafunzi, kutumia muda mwingi kutafuta maji nje ya shule, jambo ambalo licha ya kuwapotezea muda wa kujifunza, pia ni hatari kwa usalama wa wanafunzi hasa wanafunzi wa kike.

Ameongeza kuwa, barabara ya kuingia shuleni hapo ni mbovu, wakati mwingine walimu kushindwa kufika shuleni hasa kipindi cha mvua, kutokana na shule hiyo kuwa na upungufu wa nyumba za walimu na kukosekana nyumba za kupangisha kijijini hapo, jambo linalowalazimu baadhi ya walimu kuishi mjini zaidi ya Kilomita 30 kutoka shuleni hapo.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo, ameahidi kushughulika suala hilo, ili maji yaweze kupatikana shuleni hapo na kuhakikisha barabara hiyo inatengenezwa, ili kutimiza lengo la serikali la wanafunzi kupata elimu katika mazingira rafiki.

" Ninaahidi kwenda kuhughulikia suala la upatikanaji wa maji shuleni hapa, pamoja na matengenezo ya barabara ambayo hata mimi nimeiona sehemu ambayo daraja linakaribia kukatika muda wowote na  kupoteza mawasiliano na kuzuia kuingia wala kutoka" ametibitisha Naibu Waziri Waitara


Aidha mheshimiwa Waitara, amewapongeza wananchi wa maeneo hayo kwa kujitoa, kuchangia miradi ya maendeleo katika shule zao, na kuwataka kuongeza kasi na kuendeleza mabweni mawili yaliyoanzwa kujengwa na serikali ili kuongeza idadi ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika shule hizo.

Naibu Waziri huyo pia ameushauri uongozi wa halmashauri ya Arusha, kufanya mawasiliano endapo wanakutana na changamito za kifedha na kimazingira, zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi, mara baada ya serikali kutoa fedha za miradi, badala ya kufanya maamuzi ya matumizi ya fedha hizo, ili kuepuka hoja za ukaguzi.

Katika shule  hizo mbili, zaidi ya shilingi milioni  600  zimetumika kuendeleza miundombinu ya vyumba 12 vya madarasa na  mabweni ya kidato cha tano na sita, ukamilishaji wa maabara za masomo ya Sayansi, ujenzi wa Maktaba, umaliziaji na ukarabati wa mabwalo ya kulia chakula pamoja na ujenzi wa vyoo.


Naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI mheshimiwa Mwita Waitara akikagua jengo la Bwalo la kulia chakula wanafunzi wa shule ya sekondari Mwandet, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na fedha za miradi ya P4R.

Bwalo la chakula shule ya Sekondari Mwandet liko hatua za mwisho kukamilika baada ya Serikali kutoa shilingi milioni 60 fedha za P4R kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa bwalo hilo.








Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.