• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

NAIBU WAZIRI TAMISEMI MHE. NDEJEMBI AAGIZA HALMASHAURI KUKAMILISHA MIRADI KWA WAKATI

Posted on: September 30th, 2023

OR-TAMISEMI


NAIBU Wazir, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mhe. Deogratius Ndejembi amezitaka halmashauri nchini kuhakikisha zinakamilisha kwa wakati utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia mradi wa kuboresha shule za sekondari (SEQUIP) na mradi wa kuboresha shule za msingi (BOOST) ili kutumiwa  na wanafunzi watakaojiunga na shule hizo Januari, 2024.


Mhe Ndejembi ameyasema hayo kwenye ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya alipokuwa akikagua ujenzi wa shule ya msingi Muungano na Mshikamano pamoja na Shule ya Sekondari tarajiwa ya Lwanjikolwa.


Akizungumza na viongozi na wataalamu wa Halmashauri hiyo, Mhe Ndejembi amepongeza kasi nzuri ya utekelezaji wa miradi huku akizitaka halmashauri nyingine kuiga mfano wa halmashauri hiyo katika kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.


"Jitihada kubwa sana imefanywa na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kutafuta fedha hizi za maendeleo ambapo kazi yake inaonekana, sasa hatutegemei mtu yeyote arudishe nyuma jitihada hizi kubwa zinazofanywa na serikali katika kuwahudumia wananchi wetu."


"Miradi hii ya BOOST na SEQUIP tunatarajia yote ikamilike katika muda uliopangwa na ni maelekezo ya Serikali kwamba isiwepo halmashauri ambayo itashindwa kukamilisha ndani ya muda. Na siyo tu ikamilike bali thamani ya fedha iliyotumika ifanane na miradi. Hatutomchekea yeyote ambaye atashindwa kusimamia miradi hii kwa uadilifu," amesema Mhe. Ndejembi.


Mhe Ndejembi pia amezitaka kamati zinazosimamia miradi hiyo kufanya kazi kwa umoja ili kuepuka migongano ambayo husababisha kushindwa kukamilisha miradi kwa wakati lakini pia kushindwa kusimamia ufanisi wa kazi na kusababisha kuwepo kwa ubadhirifu wa fedha za umma.


Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Mhe. Oran Njeza ameishukuru serikali kwa kazi kubwa iliyofanya ya kupeleka miradi ya maendeleo ndani ya jimbo hilo huku akiahidi kushirikiana na wataalamu katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.


" Jimbo letu hili tumeletewa miradi mingi ya maendeleo hii ya elimu katika shule za msingi na sekondari ikiwemo. Tunamshukuru sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na tunaahidi kwamba tutahakikisha tunaikamilisha kwa wakati ili azma yake ya kuwahudumia wananchi wa halmashauri ya wilaya ya mbeya iweze kutimia," amesema Mbunge Njeza.


&&&




Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI MTENDAJI WA HALASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA BW. SELEMAN MSUMI AWASHONEA SARE MADEREVA WA HALMASHAURI HIYO

    October 02, 2025
  • WIZARA YA KILIMO KUPITIA MAMLAKA YA UDHIBITI WA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO (COPRA) YAZINDUA RASMI MSIMU WA UNUNUZI WA ZAO LA PARACHICHI KWA MWAKA 2025/2026

    September 27, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ARUMERU MWINYI AHMED MWINYI AHITIMISHA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT)

    September 21, 2025
  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA AWAASA WANANCHI KUJENGA UTAMADUNI WA USAFI

    September 21, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.