• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

NAIBU WAZIRI WA AFYA AMEUTAKA UONGOZI WA ARUMERU KUSAIDIA PLASTER HOUSE INAYOTOA HUDUMA YA UPASUAJI KWA WATOTO WENYE ULEMAVU

Posted on: July 23rd, 2021

Na. Elinipa Lupembe.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Dkt. Godwin Mollel, ameuagiza uongozi wa wilaya ya Arumeru, kutambua mchango unaotelewa na taasisi za dini katika sekta ya afya kwa kuweka mpango wa pamoja katika kuhudumia watoto wenye matatizo ya ulemavu nchini.

Naibu Waziri huyo, amesema hayo, alipotembela The Plaster House, inayoendeshwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzanzia Dayosisi ya Kaskazini Kati, chini ya hospitali ya Seliani Ngaramtoni, na kushudia huduma mbalimbali za upasuaji zinazotolewa kwa watoto wenye ulemavu wa viungo na kurekebishwa viungo hivyo na kuwa wazima kuendelea na maisha ya kawaida.

Nimejionea kazi inayofanyika hapa Plaster House, kazi inayofanyika ni kubwa ya kuisaidia watoto wa kitanzania wenye ulemavu kwa gharama za wafadhili,   ifike wakati sasa Serikali kuanza kufikiria namna ya kuweka mipango ya kushiriana na Plaster hii, kuwahudumia watoto wenye changamoto za ulemavu nchini, ambao wengi wao wanafichwa na kukosa haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kupata elimu." amesema Naibu Waziri huyo.

Amemtaka Mkuu wa wilaya ya Arumeru, kuangalia namna ya kuweka mipango ya kuongeza nguvu kwenye Plaster House hiyo, Plaster ambayo kimsingi inatoa huduma kubwa mno kwa wananchi wasio na uwezo kiuchumi, huduma ambayo ingepaswa kutolewa na serikali, hivyo ameagiza halmashauri kutambua umuhimu wa huduma hiyo na kuweka mkakati wa kushiriki kwa hali na mali kuisaidi utoaji wa huduma hiyo na kufikia watoto wengi zaidi wenye ulemavu.

Naye mkuu wa wilaya ya Atumeru Mhe. Mhandisi Richard Ruyango,  licha ya kuridhishwa na huduma za upasuaji zinazotolewa na Plaster House hiyo, ameupongeza na kuushukuru uongozi wa Plaster House hiyo kupitia kanisa l KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, na kuahidi kukutana na uongozi wa Kituo hicho kupanga namna ya serikali kushiriki katika kuongeza utoaji wa  huduma hiyo kupitia halmashauri ya Arusha na wadau wengine wa maendeleo.

Akielezea shughuli zinazofanya na kituo hicho Mratibu wa Mradi Aireen Ulomi, amefafanuwa kuwa The Plaster House hiyo inafanya upasuaji wa kurekebisha ulemavu wa aina mbalimbali kwa watoto wa chini ya miaka 18,  ikiwemo 'neuro surgery' kwa wenye matatizo ya migongo wazi na vichwa vikubwa,  'orthopedic surgery' kurekebisha mifupa kwa  watoto wenye matege makubwa wanaoshindwa kutembea na miguu kifundo, 'plastic surgery' kwa watoto waliopata majanga ya moto na  kusababisha ulemavu, pamoja na watoto wenye midomo sungura.

Aidha Aireen  ameongeza kuwa, huduma zote hizo zinatolewa kupitia wafadhili kutoka ndani na nje ya nchi hasa nchi za Marekani na Australia, huku wazazi wakichangia kiasi kidogo cha gharama, kwa ajili ya matibabu, ikiwa na lengo la kuweka ushirikiano kati Plaster na familia za watoto wanaopata huduma

"Plaster House ina uwezo wa kuhudumia mpaka watoto 140 kwa wakati mmoja. na kwa mwaka tunahudumia zaidi ya watoto 700, kutoka maeneo yote nchini Tanzania, katika kipindi chote cha matibabu mtoto hukaa kituoni hapa, huku akiendelea kupata huduma ya kufundishwa stadi mabalimbali ili akimaliza kutibiwa aende akaanze shule, kupitia mfumo rasmi wa elimu" ameweka wazi Mratibu huyo wa Plaster House

Aidha ameelezea licha ya mafanikio ya huduma ya matibabu wanayopata watoto, lakini pia baada ya matibabu watoto hao  huweza kumudu kuanza masomo kama watoto wengine, kutoka na ukweli kwamba jamii nyingi bado zina unyanyapaa kwa watoto walemavu, wengi wanaofika hapo wanakuwa hawajapelekwa shule kutokana na mtazamo hasi wa jamii juu ya ulemavu.

Hata hivyo imelezwa kuwa licha ya jitihada za serikali na wadau mbalimbali kushiriki kutoa huduma hizo lakini bado jamii inakabiliwa na changamoto ya kuwaficha watoto watoto wenye ulemavu na baadhi kukataa kugharamia kiasi kidogo ili kuwaleta watoto kupata huduma, na kuwaona kwamba hawana umuhimu tena katika jamii, jambo ambalo kupitia mradi huu, unawatafuta watoto hawa na kuwaelimisha wazazi katika maene yao.

Awali KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kapitia programu yake ya The Plaster House chini ya Hospitali ya Selian Ngaramtoni, imefanikiwa kutoa hudumia takribani  watoto 5,000  tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008 ikiwa na uwezo wa kuhudumia mpaka watoto 140 kwa wakati mmoja,  na wastani wa zaidi  ya watoto 700.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri, alifanya ziara katika hospitali ya mkoa wa Arusha Mount Meru, hospitali ya Lutherani Selian Hospital za jijini Arusha pamoja na Hospitali ya wilaya ya Arusha Olturumeti na hospitali ya Serilin Ngaramtoni inayosimamia kituo cha  The Plaster House na kuzungumza na watumishi wa hospitali hizo zote.







Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.