Na Elinipa Lupembe.
Mashirika yasiyo ya kiserikali 'NGOs', halmashauri ya Arusha, yametakiwa kuweka wazi miradi wanayoitekeleza kwa jamii katika maeneo husika, lengo likiwa ni kila mwananchi kufahamu miradi hiyo katika maeneo yao.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru ambaye ni Mwenyekiti ya Kamati ya Mashirika hayo, Mkuu wa Kitengo cha Sheria halmashauri ya Arusha, Monica Mwailolo wakati akifungua kikao cha kuwasilisha taarifa za Mashirika, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri hiyo, amebainisha kuwa, Serikali imeweka taratibu ambazo mashirika yanapaswa kufuata ikiwemo usajili, uwazi na uwajibikaji katika kutekeleza miradi hiyo.
Amebainisha kuwa kila shirika linalofanya kazi katika eneo husika ni lazima wananchi wa eneo hilo wapate taarifa sahihi za shirika hilo, ikiwemo shughuli zinazofanywa na endapo kuna mradi unatekelezwa, shirika liweke wazi mradi huo na gharama zake pamoja na muda wa utekelezaji wa mradi huo.
"Wananchi wanatakiwa kuzifahamu huduma mnazozitoa katika maeneo yao, hivyo ni lazima kuwafahamisha miradi mnayoitekeleza kupitia mbao za matangazo kwenye ofisi za kata na vijiji, ikionyesha muda wa kuanza mradi na kukamilika kwake ili wananchi wapate kutumia huduma mnazozitoa katika maeneo yao na si kufanya kwa siri". Amesisitiza Mwanasheria
Imeelezwa kuwa, mashirika yanapaswa kutambua, nafasi ya Msajili wa NGO's, utekelezaji wa miradi kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali, pamoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi hiyo kwa kila robo ya mwaka yaani kila baada ya miezi mitatu ya mwaka wa fedha husika.
Adha Mwenyekiti huyo ameweka wazi kuwa, Serikali inatambua na kuthamini kazi kubwa na njema inayofanywa na kashirika hayo ya kuwahudumia wananchi na jamii, kazi ambazo amekiri kuwa ni utekelezaji wa vipaumbele vya Serikali ya awamu ya sita.
Naye Mratibu Masajili wa Mashirika, halmashauri ya Arusha, Ahadi Mlai, amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za mashirika hayo lakini pia, ni kukumbushana wajibu wa mashirika hayo kwa serikali na jamii.
Hata hivyo, wawakilishi wa Mashirika hayo, licha ya kuishukuru Serikali kwa kuwapa fursa ya kushiriki katika kuihudumia jamii, wameupongeza uongozi wa halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na taasisi hizo, jambo ambalo linafanya mashirika hayo kutekeleza majukumu yao kwa wepesi.
Wameongeza kuwa, vikao vya kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi kwa kila robo ya mwaka, ni vya muhimu kwa kuwa vinawakutanisha wadau wa mashirika pamoja na kuwapa fursa ya kubadilishana uzoefu na namna ya kutatua changamoto zinazowakabili sambamba na kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa serikali na mashirika hayo.
"Tunampongeza mkurugenzi na watalamu wake, kwa kushirikiana nasi katika kutekeleza miradi yetu, kila tunapohitaji msaada tunaupata kwa wakati, na kwa kukutana kila robo ya mwaka kutaongeza tija na ufanisi katika kazi na zaidi kufikia malengo ya mashirika na ya Seikali kwa ujumla wake" Amebainisha Elia Mbanguka Mratibu wa shirika la Destiny Foundation
Naye Meneja wa shirika la Kids Care International - Tanzania, Glory Swai, amesema kuwa licha ya mafanikio makubwa ya Serikali na mashirika, bado kuna changamoto kubwa ya ukatili dhidi ya watoto, huku jamii ikiwa na hofu ya kutoa taarifa na ushirikiano wakati wa kesi za ukatili, inayotokana na mila na desturi za kabila la kimaasai.
Awali Halmsahuri ina mashirika 42 yanayofanyakazi za kuhudumia jamiii, sekta ya elimu, afya, kilimo, haki za watoto, wanawake na vijana katika maendeleo na Ustawi wa jamii.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria halmashauri ya Arusha, Monica Mwailolo wakati akifungua kikao cha kuwasilisha taarifa za Mashirika, kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru ambaye ni Mwenyekiti ya Kamati ya Mashirika hayo, kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Ausha.
Msajili Msaidizi wa NGO's halmashauri ya Arusha, Ahadi Mlai akitoa ufafanuzi wa uwasilishaji wa taarifa za mashirika, wakati wa kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Ausha.
Mwakilishi wa shirika la CWCD akiwasilisha taarifa ya shirika lake, wakati wa kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Ausha.
Mwakilishi wa shirika la Kids Care International - Tanzania, Glory Swai, akiwasilisha taarifa ya shirika lake, wakati wa kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Ausha.
Wawakilishi wa Mashirikia wakifuatilia mijadala mbalimbali wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa za mashirika yasiyo ya kiserikali, kwenye ukumbi wa mikutano, halmashauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.