Na Elinipa Lupembe
Benki ya NMB kanda ya Kaskazini, imeahidi kuendelea kuboresha na kudumisha ushirikiano baina yake na halmashauri ya Arusha, katika kutekeleza shughuli mbalimbali za kibenki na za kijamii, lengo likiwa ni kusogeza huduma karibu na wananchi.
Makubaliano hayo yamefanyika wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha pamoja mameneja wa matawi ya NMB Arusha na Wakuu wa Idara na vitengo, halmashauri ya Arusha, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Palace Hotel Arusha jijini Arusha.
Mameneja hao, wamepata wasaa wa kuelezea fursa mbalimbali za kibiashara na kijamii zinazotolewa na benki hiyo , wakijipambanua zaidi ya kuweka, kutoa na kukopa fedha, huduma ambazo ni pamoja na ushauri wa kibiashara na uwekezaji kwa wafanyabiashara binafsi, mashirika, kampuni na hata Taasisi za serikali ikiwemo halmashauri.
Meneja wa NMB tawi la Clock Tower, Emmanuel Kishosha, amewataka watalamu hao wa halmashauri, kushirikiana na watalamu wa benki kwa kutumia fursa hizo kulingana na huduma zinazotolewa na mahitaji ya halmashauri lengo likiwa ni kufikia malengo ya serikali ya kuwahudumia watanzania.
"NMB inahudumia watumishi mmoja mmoja, lakini pia inatoa huduma nyingine nyingi kwa taasisi, inatoa huduma kwa vikundi vya wakulima, wafugaji, wajasiriamali pamoja na kutumia 1% ya faida yake kuirudisha kwenye jamii kwa kutoa misaada katika sekta ya Elimu na Afya ambayo inakwenda moja kwa moja kwa wananchi katika halmashauri zenu" Ameweka wazi Kishosha.
Hata hivyo watalam wa halmashauri ya Arusha, licha ya kuushukuru uongozi wa benki hiyo, wamekiri kupata uelewa wa ziada wa huduma zinazotolewa na benki hizo, huduma ambazo hawakuzifahamu hapo awali na kuahidi kushirikiana na benki hiyo kwa kutumia fursa zilizopo.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, ameweka wazi kuridhishwa na huduma zinazotolewa na benki hiyo na kuitaka benki hiyo kukaribia na kuwekeza kwenye halmashauri hiyo, kutokana na kuwa na maeneo ya uwekezaji ambayo yatawezesha kurahisisha huduma kwa wananchi wa halmashauri hiyo.
"Licha ya kwamba mnatoa huduma kupitia asilimia 1 ya faida, lakini tuwaombe kupitia kitengo cha uwekezaji, kuwekeza katika Halmashauri yetu, kwa kuwa kuna maeneo ambayo yanafaa kwa uwekezaji, jambo ambalo litawezesha halmashauri kupata manufa na benki kupata faida
Kikao kazi hicho kimefungua ufahamu kwa watumishi juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo, huku kwa pamoja wakikubaliana kushirikiana hata katika shughuli za kibenka na zile za kijamii.
SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI
JIANDAE KUHESABIWA 23.08.2022
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.