PPRA KANDA YA KASKAZINI YAENDESHA MAFUNZO YA MFUMO WA UNUNUZI WA UMMA (NeST) KWA WADAU MBALIMBALI HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Omar Sembe amewataka washiriki wa mafunzo ya mfumo mpya wa manunuzi ya umma ( Nest) kuyatumia mafunzo hayo vyema ili kuleta tija mahali pa kazi.
Bwana Sembe ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku mmoja yaliyoandaliwa na PPRA kanda ya kaskazini kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi wanaoshughulika na mifumo ya manunuzi ya Serikali ndani ya Halmashauri ya Wilaya Arusha.
Akieleza dhima nzima ya mafunzo hayo, Afisa wa PPRA kanda ya kaskazinii Bi. Nuru Bazaar amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwafikia wadau moja kwa moja na kutatua changamoto zao wanazokutana nazo wanapokuwa wakitumia mfumo wa ununuzi wa umma (NeST).
Bi.Nuru amesema kuwa watumishi wa Umma wasiogope kutumia mfumo huu kwani teknolojia inakuwa kwa kasi duniani na mifumo mingi hubadilika kila wakati na ni sharti la kukubali kuendana na wakati.
Kwa upande wake, bi Diana Tatala mkufunzi wa mafunzo hayo amewasisitiza wadau kufanya makisio halisi kwa kuzingatia jiografia ya eneo husika ambapo mradi unatekelezwa. “Thamani halisi ya kile kinachojengwa/Kinachonunuliwa lazima ionekane,gharama za miradi ziende sambamba na gharama za usimamizi wa miradi hiyo,huwezi kuwa na mradi usio na gharama za usimamizi".amesema Bi. Diana Tatala
Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika katika ukumbi wa shule ya Green Acres yamegusa makundi mbalimbali ya wadau wa mfumo wa ununuzi wa umma wakiwemo,Waganga wafawidhi,Walimu wakuu,Wakuu wa shule,Watendaji wa Kata,Wakuu wa Divisheni na Vitengo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.