Timu ya utekelezaji wa mradi wa Tupange Pamoja, wameendelea na kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa mradi huo kwa kipindi cha robo mbili za mwaka wa fedha 2020/2021.
Katika kikao kazi hichi, timu hiyo imejipanga kuendelea kukabiliana na kutatua changamoto zinazoikabili jamii juu ya Elimu ya Uzazi na Uzazi wa Mpango, na kuwejiwekea mikakati thabiti ya kumalizia robo mbili zilizobaki za mwaka huu wa fedha unaoendelea.
Mradi wa TCI -Tupange Pamoja unashughulika na kutoa Elimu kwa jamii, ikiwa ni pamoja na Elimu ya Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango pamoja na Afya ya Uzazi kwa Vijana.
Aidha mradi huu, unatekelezwa na halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na Shirika la JHPIEGO kupitia mradi wake wa TCI- Tupange Pamoja kwa ufadhili wa Taasisi ya Bill&Melindagate ya nchini Marekani.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.