Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Raisi wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Ruto mara baada ya mazungumzo yao nchini Kenya leo Septemba 13, 2022.
Hata hivyo Mhe. Samia ameshiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais Rutto na kuwapongeza wakenya wote kwa ukomavu wa demokrasia waliouonyesha wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.
"Ndugu zetu wakenya kama kuna zawadi mliyoitoa kwa Jumuia ya Afrika Mashariki mwaka huu ni zawadi ya amani mliyoiweka katika uchaguzi, tunawashukuru sana sana" . Amesisistiza Mhe, Rais Mama Samia
Rais wa mpya wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. Ruto ameapishwa leo mara baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 9, 2022 na kuwa Rais wa awamu ya tanokuiongoz nchi hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.