RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANUA NA AMIRI JESHI MKUU,DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA SALAMU ZA POLE KWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI JENERALI JOCOB MKUNDA KUFUATIA KIFO CHA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI MSTAAFU, JENERALI DAVUD B. MUSUGURI.
Kwaheri, Jenerali.
Ninatoa salamu za pole kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda, Makamanda, wapiganaji wastaafu, wapiganaji walio katika utumishi, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa kuondokewa na shujaa wetu, mpendwa wetu, mwalimu, mshauri na kiongozi wetu, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali (Mstaafu) David Bugozi Musuguri.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha yake ya miaka 104, ambapo miaka 46 kati ya hiyo ameitumikia nchi yetu kwa weledi, umahiri, kujituma, ushujaa, nidhamu na kwa mafanikio ya hali ya juu, akiishi kiapo chake cha kuwa tayari kuutoa uhai wake ajili ya ulinzi wa Taifa letu. Ametuachia mfano bora wa utumishi wa umma utakaoendelea kuwa mwanga ndani na nje ya Majeshi yetu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.