• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RAS MKOA WA ARUSHA ATETA NA WATUMISHI ARUSHA DC; AWATAKA KUFANYAKAZI KWA WELEDI NA UADILIFU

Posted on: October 10th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Katibu Tawala mkoa wa Arusha Massaile Albano Musa amewata watumishi kufanyakazi kwa weledi kwa kwa kuzingatia kanuni sheria na taratibu za utumishi wa Umma kwa kuachana na vitendo viovu ambavyo ni kinyume na maadili na taratibu za kazi .

Katibu Tawala huyo amesema hayo wakati wa kikao kazi, kilichowakutanisha watumishi wa sekta zote chenye lengo la kusikiliza kero za watumishi sambamba na kuwambushana utekelezaji bora wa majukumu ya kazi katika kuwatumikia wananchi.

Amewasisitiza watumishi kuwa, wanalo jukumu kubwa la kuwahudumia wanachi kwa niaba ya serikali hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu,  kuwa na nidhamu katika kazi pamoja na kutunza siri za serikali kwa kufuata maelekezo ya viongozi kwa kuzingatia kanununi, sheria, miongozo na taratibu za utumishi wa Umma.

"Fanyenyeni kazi kwa  upendo, shirikianeni, heshimianeni kwa  kutambua umuhimu wa kila mtu kwa nafasi yake ili kufikia malengo ya serikali ya awamu ya sita ya kuwahudumia wananchi, serikali imewaamini, rudisheni fadhila kwa wananchi" Amesema Katibu Tawala huyo

Aidha ameutaka uongozi wa halmashauri kuimarisha mahusiano bora kazini kwa kusimamia stahiki na maslahi ya watumishi ikiwemo malipo ya likizo, stahiki za wagonjw,  wastaafu pamoja na malipo ya uhamisho bila kujali nani ni nani.

"Idara ya utawala simamieni Maafisa Watendaji wa kata na vijiji kuhakikisja wanafanya vikao na mikutano ya kisheria ngazi za vijiji na kata, kwa kila robo ya mwaka na kuwasilisha mihtasari ya vikao na mikutano ofisi ya mkurugenzi" Amesema

Pia amewataka Maafisa Elimu kata kuzingatia usimamizi wa sekta ya elimu katika shule, licha ya kusimamia taaluma shuleni zaidi kusimamia ulinzi na usala wa mtoto kuanzia nyumbani mpaka shuleni, upatikanaji wa chakula cha mchana kwa wanfunzi.

Hata hivyo watumishi wa halmashauri ya Arusha wamemshukuru Katibu Tawala kwa kufanya kikao pamoja nao, kikao ambao licha ya kutoa kero zao kimewakumbusha majukumu yao ya kazi na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa ili kufikia lengo la serikali la kuwahudumia wananchi.

Afisa Tarafa ya Mukulat Tatu Furaisha, amemshukuru RAS kwa kikao kazi hicho na kusema kuwa kiongozi anapokutana na watumishi ni afya katika kazi na kuahidi kufanyia kazi malekezo yote ikiwemo nidhamu ya kazi.

Naye Katibu Tawala Arumeru Joseph Mabiti, ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa hususani katika kata na vijiji kwa kuhakikisha vikao na mikutano ya kisheria inafanyika kwa wakati  ili kuongeza uwazi wa shughuli za serikali kwa maendeleo ya wananchi.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, amethibistisha kupokea maelekezo na kuendelea kuwasimamia watumishi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Kanuni, Sheria na taratibu huku akiahidi kuendela kutoa stahiki za watumishi kwa kuzingatia taratibu za utumishi wa Umma.


ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.