Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongela amewaapisha wakuu wanne wateule wa wilaya za mkoa wa Arusha, walioteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu huyo wa mkoa amewataka wakuu hao wa wilaya kwenda kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi katika maeneo yao huku wakizingatia sheria kanunu, taratibu na hekima.
Mheshimiwa Mongela amewasisitiza wakuu hao wa wilaya kuwa kiapo hicho cha Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kinawalazimu kutumia sheria kanuni na taratibu pamoja na hekima katika kutekeleza majukumu yao yakiutendaji.
"Suala la ulinzi na usalama ni la kipaumbele cha kwanza kwenu wakuu wa wilaya, tambueni kuwa hakuna maendeleo pasipokuwa na usalama kwa wananchi, mnalo jukumu kubwa la kusimamia ulizni na usalama katika maeneo yenu". Amesisitiza Mhe. Mongela
Aidha amewaagiza kusimamia na kuhakikisha watoto wote walioandikishwa kuanza darasa la awali nala kwanza, pamoja na wale wa kidato cha kwanza kuhakikisha wanaripoti kwenye shule walizopangiwa haraka iwezekanavyo.
Amewakumbusha kuwa Agenda ya kitaifa ya utunzaji wa mazingira, na kuwataka kuhakikisha kila wilaya inatumia msimu huu wa mvua kupanda miti katika maeneo yao ya kazi kwa kushirikiana na TFS.
Awali wakuu hoa wa wolaya wameapishwa mara baada ya kueuliwa na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuzihudumi wailya za Arumeru, Arusha, Longido na Monduli.
"ARUSHA DC Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#KaziInaendelea✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.