• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RC Gambo awataka Maafisa Watendaji kata na vijiji Arumeru, kugawa vitambulisho kwa wajasiriamali wote

Posted on: February 6th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, mheshimiwa Mrisho Gambo, amewataka Maafisa Watendaji wa Kata na vijiji, wilayani Arumeru kulipa umuhimu zoezi la ugawaji vitambulisho vya wajasiriamali, alipokutana nao kwenye ukumbi wa mikutano, halmashauri ya Arusha.

Mkuu huyo wa mkoa, ametoa wito huo alipokutana na watendaji hao wa halmashauri za Arusha na  Meru zinazounda wilaya ya Arumeru na kuwakabidhi jumla ya vitambulisho elfu 24 kupitia Mkuu wa wilaya ya Arumeru,  na kutoa muda wa mwezi mmoja, kuhakikisha wajasiriamali wote katika maeneo yao wamepata vitambulisho hivyo.

Mheshimiwa Gambo ametoa ufafanuzi,  juu ya umuhimi wa zoezi hilo na kusema kuwa, lengo la serikali ni kutambua idadi ya wajasiriamali walio katika sekta isiyo rasm,  kutokana na ukweli kuwa, wafanya biashara wengi wanakwepa kulipa kodi huku wafanya biashara wachache wakibeba mzigo wa kulipa kodi kila mwaka.

Kupitia vitambulisho hivyo, kutawezesha  kutambulika kwa wajasiriamali walio katika sekta isiyo rasmi, kuweza kuwasimamia wajasiriamali hao kukua kwa kukuza mitaji ili na kuwawezesha kufikia ngazi ya wafanyabiashara.

"Wapo wafanyabiashara wasiojulikana popote, lipo kundi la wafanyabiashara limejificha, wao hawalipi  kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA wala kulipa halmashauri, kupitia zoezi hili la utambuzi, serikali itawapata hao wanaojificha" amesema mheshimiwa Gambo.

Licha ya kuwa serikali imeweka mkakati wa kulitambua kundi hilo la wajasiriamali kwa kuwapa vitambulisho, lakini kumekuwa na upotoshaji juu ya vitambulisho hivyo, unaosababisha jamii kutokuelewa lengo la serikali la kugawa vutambulisho hivyo, na kushindwa kupima ni yupi mfanyabiashara na yupi ni mjasiriamali.

Hata hivyo Gambo amewata watendaji hao, kuhakikisha wajasiriamali wote katika maeneo yao, wanapatiwa  vitambulisho ili kila mjasiriamali aweze kutambulika na kuweza kufanyabiashara yake kihalali bila kubughudhiwa.

"Niwatake watendaji msikae ofisini kusubiri wajasiriamali kuwafuata bali wafuateni kwenye maeneo yao na kuwasajili ili kufikia lengo la serikali  la kupata data base ya wafanyabiashara wote" amesisitiza mkuu huyo wa Mkoa.

Aidha amewataka Maafisa watendaji hao, kukusanya kodi ya majengo 'propert tax' ambayo serikali imeelekeza kila nyumba ya kawaida shilingi elfu 10 na ghorofa shilingi elfu 50, na kuagiza kila Afisa mtendaji wa kijiji kuorodhesha idadi ya nyumba katika kijiji chake ili kodi hizo zikusanywe na kupeleka TRA.

Naye Mkuu wa wilaya ya Arumeru, mhe. Jerry Muro, ameeleza kuwa kwa awamu ya kwanza wilaya ya Arumeru imeshagawa vitambulisho 4500 kati ya 6000 kupitia maafisa biashara wa halmashauri ya Arusha na Meru,  na kuonekana bado juhudi zinahitajika ili kuwafikia wajasriamali katika maeneo yao.

Hata Maafisa Watendaji hao wa kata na vijiji wamegawana vitambulisho hivyo, kulingana na idadi ya watu katika makazi, huku wale wa maeneo ya miji yakipatiwa idadi kubwa ya vitambulisho hivyo na kuahidi kwenda kuchapa kazi kwa kuwazungukia wajasiriamali katika maeneo yao.

Afisa Mtendaji kata ya Ngarenanyuki, Victor Kaijage amesema wakotayari kuanza rasmi zoezi hilo na kuahidi kufanya jitihada ili kuwafikia wajasiriamali wote katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kuwatembelea katika biashara zao ili kufikia lengo la serekali.

Wilaya ya Arumeru ina halmashauri mbili za Arusha na Meru ikiwa na kata 53 na vijiji, yenye jumla ya wakazi 591,342 kulingana na Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 na ongezeko la asilimia 2.5, huku ikiwa pia na Mamlaka mbili za miji midogo USa na Ngaramtoni, miji inayokua kwa kasi.









Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.