Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kenani Labani Kihongosi leo Alhamisi Agosti 21, 2025 amejumuika na wananchi wa Mkoa wa Arusha kwenye mazoezi ya Viungo (Jogging) iliyofanyika mapema leo asubuhi, ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa Tamasha la Tanzania Samia Connect, tamasha lililoasisiwa na kuratibiwa na Mhe. Kihongosi kusherehekea mafanikio yaliyopatikana Mkoani Arusha kwenye Miaka minne ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Tanzania Samia Connect inafanyika kwenye viwanja vya Mgambo Mkoani hapa ambapo kando ya kusherehekea miaka minne ya Rais Samia, Tamasha hilo pia linatumika kutoa huduma bure kwa wananchi ikiwemo vipimo na matibabu kwa magonjwa ya macho na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari na shinikizo la damu, huku zaidi ya miwani 3,000 zikitolewa bure kwa watakaobainika kuwa na magonjwa yenye kuhitaji miwani.
Aidha kulingana na Mhe. Kihongosi huduma nyingine zitakazopatikana katika Viwanja vya Mgambo, Uzunguni Jijini Arusha kuanzia leo mpaka siku ya kilele Agosti 23, 2025 ni pamoja na utoaji wa hati za ardhi, vitambulisho vya taifa, vitambulisho vya uraia pamoja na huduma nyinginezo ikiwemo ukaguzi bure wa magari na huduma nyingine zinazotolewa na serikali, mashirika, Taasisi zake na sekta binafsi nchini, huku pia ikiwa ni fursa kwa wajasiriamali wadogo kuuza bidhaa zao mbalimbali ikiwemo vyakula na kadhalika.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.