Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Kenan Laban Kihongosi @kenanikihongosi amepokea Mwenge wa Uhuru 2025, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu kwenye Kijiji cha Malula eneo la King'ori Kibaoni, Wilaya ya Arumeru, asubuhi ya leo Julai 05 , 2025.
Mhe. Kihongosi ameweka wazi kuwa, katika Mkoa wa Arusha, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa Km 1,203.17 kwenye Wilaya 6 na Halmashauri 7 za mkoa wa Arusha na kupitia jumla ya miradi 54 Kisekta yenye thamani ya Shilingi Bilioni 30.3.
Aidha, Katika miradi hiyo 54, miradi 18 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 12 itawekewa mawe ya msingi, miradi 4 yenye thamani ya Shilingi milioni 378.2 itafunguliwa, miradi 19 yenye thamani ya shilingi Bilioni 15.2 itazinduliwa na miradi 13 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6 itatembelewa.
Hata hivyo Mhe. Kihongosi amemkabidhi Mwenge huo wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Mwinyi Ahmed Mwinyi @m.a._mwinyi , ambapo katika wilaya hiyo Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwenye halmashauri mbili ukianzia katika katika Halmashauri ya Meru siku ya leo na kesho Julai 06, 2025 Halmashauri ya Arusha.
KAULI MBIU: "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kwa Amani na Utulivu"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.