Na. Elinipa Lupembe.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, mheshimiwa Idd Kimanta, amewaongoza wakazi wa mkoa wa Arusha na vitongoji vyake, kuuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, marehemu Richard Kwitega, shughuli iliyofanyika mapema leo, kwenye uwanja wa Sheik Amri Abeid jijini Arusha.
Akitoa salamu za rambirambi mbele maelfu ya waombelezaji, wakiwemo wafanyakazi wa Idara na Taasisis malimbali za mkoa wa Arusha na mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Mkuu huyo wa mkoa, licha ya kuhuzunishwa sana, na kifo cha Bwana Kwitega, amewataka waombolezaji hao kuyaishi matendo mema, aliyoyaishi marehemu Kwitega wakati wa uhai wake, kwa kudumisha upendo na ushirikiano mahala pa kazi.
Mheshimiwa Kimanta, amemuelezea Marehemu Kwitega, kuwa alikuwa ni mwenye mahusiana mazuri ya kikazi na kijamii katika eneo la kazi na kuongeza kuwa alikuwa ni kiungo na mhimili imara kati ya watumishi wa serikali, sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserika pamoja na vyama vya siasa na daima alihakikisha shughuli na mipango yote ya serikali inatekelezeka ndani ya mkoa wa Arusha kwa mafanikio makubwa sana katika sekta zote.
Kama nii kipuri cha gari, Kwitega niliweza kumuita 'shokomzoba', alikuwa ni mhimili wa shughuli zote za mkoa wa Arusha, aliyefanyakazi bila kuchoka, bila ubaguzi, bila majungu na kumuheshimu mkubwa kwa mdogo. ninasema tangulia Richard, tangulia Richard, hii ni kazi ya Mungu, tunaamini na sisi tuko nyuma yako" Amesisitiza Mkuu wa mkoa kwa uchungu mkubwa.
Marehemu Richard Kwitwega, amefariki kwa ajali ya gari siku ya Jumatano tarehe 03.02.2021, eneo la Mdorli -Babati mkoani Manyara, akiwa njiani kuelekea mkoani Dodoma na mwili wake unasafirishwa leo kuelekea mkaoni Mwanza wilaya ya Sengerema kwa mazishi yatakayofanyika siku ya Jumamosi.
VITA UMEPIGANA NA KAZI UMEMALIZA, TANGULIA KWITEGA TUKO NYUAMYAKO.
PICHA ZA MATUKIO UWANJA WA SHEIK AMRI ABEID- JIJINI ARUSHA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.