RC MAKONDA AHIMIZA WAFANYABIASHARA ARUSHA KUTUMIA VYEMA FURSA ZA UGENI WA MIKUTANO KATIKA KUKUZA UCHUMI
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewataka Wafanyabiashara wa Arusha kutumia vyema fursa za Mikutano mbalimbali ya Kimataifa na Kitaifa katika kuongeza mnyororo wa thamani wa kukuza Uchumi wa Mkoa.
Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo Agosti 29, 2024 wakati wa halfa ya nyama choma aliyoiandaa kwa Wenyeviti wa Bodi za Taasisi, Watendaji wa Kuu wa Taasisi pamoja na Mashirika na Wakala za Serikali iliyowakutanisha na Wafanyabiashara mbalimbali wa Arusha.
Makonda ametumia fursa hiyo ikiwa ni adhma yake ya kuifanya Arusha kuendelea kuwa kitovu cha Utalii hasa wa Mikutano pamoja na kuendelea kuvutia Wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kuweka katikasekta za Utalii,Viwanda,Michezo,Madini,Kilimo pamoja na Mahoteli.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.