RC MAKONDA AIPONGEZA SAFARI FIELD CHALLENGE – AWATAKA WATANZANIA KUIUNGA MKONO SEKTA YA UTALII
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, leo Aprili 16, 2025 amekutana na timu ya washiriki na waandaaji wa ‘Safari Field Challenge’ katika ofisi yake kwa ajili ya kusalimiana na kubadilishana mawazo kuhusu mchango wa mashindano hayo katika kukuza sekta ya utalii nchini.
Mhe. Makonda ameipongeza timu hiyo inayojumuisha majaji, washiriki na watangazaji kwa kuanzisha wazo bunifu ambalo linalenga kuinua heshima ya sekta ya Utalii na kuinua uchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kupitia sekta hiyo.
“Niwatie moyo muendelee kuifanya kazi hii nzuri, na niwaombe muendeleze sifa ya ukarimu kwa wageni wanaokuja nchini. Waongoza watalii ni watu muhimu sana katika Mkoa wetu wa Arusha, kwani hata Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha mfano mzuri katika kuithwataliiekta hii." amesema Mhe. Makonda.
‘Safari Field Challenge’ imeanza rasmi awamu yake ya kwanza kuanzia tarehe 1 hadi 16 Aprili, 2025 katika hifadhi ya Taifa ya Makuyuni na Tarangire na mashindano hayo yamekusudiwa kuibua vipaji bora vya waongozaji watalii na kutoa nafasi kwa wananchi kuwachagua waongozaji bora wa mwaka 2025 wenye Leseni ya kuongoza watalii.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.