posted by Ambrose Rashid
Maafisa watendaji wa Kata zote wametakiwa kuijua miradi yote inayotekelezwa kwenye maeneo yao, ahadi za Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa 2020/25 kwenye maeneo yao pamoja na kuelewa tija ya miradi husika kwa wanufaika wa miradi hiyo ya maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Juni 04, 2024 wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Mateves wilayani Arumeru, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Mhe.Mkuu wa Mkoa ametoa tahadhari hiyo wakati huu akijiandaa kuanza ziara ya Kata zote za Mkoa wa Arusha na kueleza kuwa atakagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Kata zote za Mkoa pamoja na kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Mhe. Makonda ametoa angalizo hilo mara baada ya kukerwa na uwajibikaji na ufanisi mdogo wa baadhi wa watendaji wa serikali za mitaa na vijiji akisema kuwa baadhi yao wamekosa sifa za kuwatumikia wananchi kutokana na uwajibikaji mdogo kwenye vituo vyao vya kazi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.