• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RC MONGELA AAGIZA; ZOEZI LA UBOMOAJI NYUMBA BARABARA YA MIANZINI - TIMBOLO, MWISHO DISEMBA 26, 2022.

Posted on: November 16th, 2022

Na Elinipa Lupembe

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela ameagiza waliojenga nyumba ndani ya mita 10 za barabara ya Mianzini , Timbolo, Sambasha hadi Ngaramtoni,  kubomoa nyumba zote hizo, kabla ya tarehe 26, Desemba 2022, ili kupisha ujenzi wa barabara unaoendelea.

Mkuu huyo wa mkao ametoa kauli hiyo alipotembela na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa Km 18, inayojengwa kwa kiwango cha lami, mradi unaotekelezwa katika halmashauri za Jiji la Arusha na Arusha, utakaogharimu shilingi bilioni 22 hadi kukamilika kwake na kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 8.

Mongella amefafanua  kuwa kwa mujibu wa sheria ya barabara ya mwaka 2007 upana wa barabara ulitakiwa kuwa mita 20 kila upande, lakini serikali ya Rais Samia inayowajali wananchi wake na haitaki wapate kero hivyo imepunguza na kuwa mita 10 kwa kila upande.

Aidha amewataka wananchi wa maeneo ambayo barabara hiyo inapita, kutoa ushirikiano ikiwa ni kuunga Mkono juhudi za serikali kwa kuwa barabara hiyo inaleta maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

"Serikali imeshaleta fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii, haiwezekani ikacheleweshwa na watu wachache wasiotaka kubomoa nyumba zao, wananchi changamkieni fursa hiyo, kuna fursa pia ya ajira wakati ujenzi huu unavyoendelea " Amesema mkuu wa mkoa huyo.

Aidha, ameitaka Wakala wa barabara Tanzania (TANROAD) kuendelea kutoa elimu ya sheria ya barabara kwa wananchi ili waweze kuifahamu vizuri na kujenga uelewa wa pamoja.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Arusha Muhandisi Regnand Massawe amesema barabara hiyo ya Mianzini Sambasha ina urefu wa KM 12 na ile inayoanzia Olemringaringa hadi Ngaramtoni ina urefu wa KM 6 na kufanya jumla ya Km 18 na ujenzi unatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti 2023.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wameishukuru serikali kwa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami na kuitaka serikali kusimamia sheria kwa usawa ili kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo bila vikwazo.

"Serikali isimamie sheria kwa watu wote, wananchi tunataka maendeleo, hao wachache wanaokwamisha wachukuliwe hatua, ili wapishe ujenzi wa barabara uendelee, tumesubiri lami kwa muda mrefu, wakati umefika sasa". Amesema  Zelote Aloyce mkazi wa Mianzini

Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa ya kukagua ujenzi wa barabara ya Mianzini, Timbolo - Kinyaki  hadi Ngaramtoni ilikuwa na lengo la kukagua ujenzi pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi wa maeneo hayo.


ARUSHA DC

KaziIendelee✍











Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.