Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella ametembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa mabweni shule ya sekondari Mringa, mradi unaotekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 260 kupitia mradi wa kuboresha miundombinu ya shule za sekondari (SEQUIP)
Licha ya kuridhishwa na utekelezaji wa Mradi ambao uko kwenye hatua ya kupaua, Mkuu huyo wa mkoa ameshauri pia kuzingatia matumizi ya mbao bora zilizokauka ili kuepuka kupinda huku akiendelea kuwasisitiza watalamu kuendelea kuzingatia hali ya ubora wa ujenzi unaofuata hatua na taratibu ili mradi ukamilike kwa wakati ukiwa na ubora unaozingatia thamani ya fedha iliyotolewa na serikali
Amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imejikita katika kuboresha miundombinu kwenye sekta ya elimu,kwa lengo la kuhakikisha watoto wa kitanzania wanasoma kwenye mazingira rafiki ili waweze kutimiza ndoto zao.
"Tunamshukuru Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuotoa fedha nyingi za ujenzi wa miundombinu ya shule, mama Samia amrona kuna umuhimu mkubwa wa kuboresha miundombinu ya shule za Serikali, ili watoto wa kitanzania wapate elimu kama watoto wengine wanaosoma kwenye shule za binafsi" Amefafanua Mhe. Mongella.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mkuu wa shule ya sekondari Mringa, amesema kuwa, wamepkea jumla ya shilingi milioni 360 kutoka serikali kuu, huku milioni 260 zikitumika kujenga mabweni mawili mapya na milioni 100 zikitumika kukarabati mabweni manne ya zamani.
Mkuu huyo wa mkoa, atafanya ziara ya siku mbili 19 - 20.09.2023 ya kukagaua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya Elimu sekondari na Msingi, miundombinu ya barabara na maji, pamoja na kufanya mikutano ya hadhara na kusikiliza kero za wananchi katika kata za Oldonyowas na Bwawani.
Arusha DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.